Friday, August 29, 2008
IJUE KAROTI NA FAIDA ZAKE
Wednesday, August 27, 2008
JE, NITAKULA NINI AU UTAKULA NINI NA KWA KIASI GANI?
- Unashauriwa ule kwa wingi vyakula vya nafaka kama wali, ugali, mkate n.k, ingawa hapa watu wengine hawataki kabisa kusikia habari za ugali labda wale watu waliokulia bara.
- Kula kwa wingi vyakula vya mbogamboga na matunda maana yakula hivi vina virutubisho vyote na ni kinga na dawa kwa baadhi ya maradhi mwilini .
- Kula kwa kiasi kidogo vyakula vyenye protini nyingi hasa vile vinavyotokana na mazao ya wanyama kama vile; nyama, kuku, mayai, maziwa, mtindi, samaki na maharage makavu n.k, ukiweza kula vyakula vya aina hii mara moja kwa wiki.
- Ukiweza, acha kabisa ama kula kidogo sana vyakula vyenye asili ya mafuta ama vilivyoongezwa mafuta, vilivyoongezwa sukari. Najua wengi wanapenda kula vyakula vilivyokaangizwa, ukiwaambia wapike ama wale chukuchuku wanakujibu kwani nina shida gani, raha jipe mwenyewe, kumbe hawajui ndiyo kwanza wanatengeneza shida zitakazowapa karaha badala ya raha.
Najua ni vigumu kwa watu kufuata mpangilio huu. Lakini kama umedhamiria kuilinda afya yako unaweza na tena vyakula hivyo ni rahisi kuvipata katika masoko yetu hapa nchini TZ tofauti na wenzetu kule majuu.
Aidha niliposema kula kulingana na mahitaji ya mwili wako, unapaswa kujua wewe mwenyewe unafanya shughuli gani. Kwasababu, mahitaji ya miili yanatofautiana kulingana na aina ya shughuli au kazi ya mtu husika. Kwa mfano watu wanaofanya kazi maofisini na walimu wanahitaji kiasi kidogo cha chakula; kwa wanafunzi na wafanyabiashara na wachuuzi pamoja na watumishi wa kazi za ndani wanahitaji nyongeza kidogo tofauti na mtu wa ofisini; mafundi kama seremala, umeme, watumishi wa nyumbani wanaofanya kazi kama za kulisha mifugo na nyingine ngumu wanahitaji chakula cha kutosha; na wafanyakazi wa ujenzi kama wabeba zege, ujenzi wa barabara, migodini, wanariadha na wengine wa aina hiyo wanahitaji chakula kingi ili kutosheleza mahitaji ya miili yao kwani wao wanatumia calories nyingi. Hivyo ni vema ukazingatia hilo ili usije kula chakula zaidi ya mahitaji ya mwili wako na matokeo yake ni unene unaoweza kukusababishia matatizo au hata usipokuwa mnene unaweza kujikuta unapata kisukari kinyume na matarajio yako.
Kwa maelezo hayo nadhani nitakuwa nimejibu baadhi ya maswali ya wasomaji waliotaka kujua watakula nini, kwa kiasi na kiwango gani na wakati gani. Kumbuka, hapo baadaye nitakupa jinsi unavyotakiwa kupangilia milo yako kwa siku. Kama una maswali zaidi usisite kuuliza.
Asante kwa ushirikiano wenu na karibu tena.
Tuesday, August 26, 2008
DOKEZO JUU YA MANENO "EAT AT YOUR OWN RISK"
UMEWAHI KUONA MAANDISHI HAYA MAHALA POPOTE?
EAT AT YOUR OWN RISK
2FLAG
Monday, August 25, 2008
UNAFAHAMU NAMNA UNAVYOWEZA KULA TUNDA LA AVOCADO
- fruit salad, yaani mchanganyiko wa matunda mbalimbali yaliyoandaliwa kwa kukatwakatwa vipande vidogo na kukamuliwa limao kwa ajili ya kuongeza ladha. Maandalizi ya mchanganyiko huu ni rahisi kwani muandaaji anatakiwa kuchukua avocado na matunda mengine kama vile ndizi, matango, mapapai, zabibu n.k na kisha kuyaosha na kuyamenya ambapo mchanganyiko huo unaweza kuhifadhiwa kwenye jokofu ili upate ubaridi kidogo kabla ya kuliwa. mchanganyiko huu pia unaweza kuongezwa maziwa kama utapenda
- Vegetable salad, huu ni mchanganyiko wa avocado na jamii ya mbogamboga zilizoandaliwa kwa kukatwakatwa vipande. Mchanganyiko huu unaweza kuhusisha mboga kama nyanya, cabbage, pilipili hoho, n.k. Pia katika mchanganyiko kama huu unaweza kuweka limao ili kuleta ladha fulani mdomoni. Kwa wenzetu hupenda kuweka aina fulani ya mafuta kama vile olive oil ili kuipa ladha zaidi. Lakini kama uwezo wetu hauruhusu mambo hayo basi siyo lazima sana kwani vitu vya msingi utakuwa umevipata. Maandalizi yake hayana tofauti na yale ya fruit salad.
- Juisi, tunda la avocado ni zuri kwa kutengenezea juisi. Inashauriwa upate avocado lililoiva vizuri ili iwe rahisi kulisaga. Unaweza kutengeneza juisi ya avocado pekee au unaweza kuchanganya na tunda jingine kama vile apple, pensheni, embe n.k. Utengenezaji wa juisi unategemea uwepo wa vifaa kama juicer au blenda. Lakini kama hauna uwezo wa kupata au kununua vitu hivyo ambavyo pia vinatumia umeme, unaweza kutumia kinu kidogo kusaga ili kupata mchanganyiko uliosagika vizuri kisha kupata juisi uliyoikusudia. Wakati mwingine inabidi tukumbuke tulikotoka ambapo wazee wetu walikuwa wanatengeneza dawa za aina hiyo kwa kutumia vifaa hivyo vya asili.
- Fresh fruit, unaweza kula avocado kama lilivyo kwa kulimenya na kuondoa mbegu yake. Lakini zingatia usafi kabla ya kula tunda hilo usije ukapatwa na maradhi ya tumbo.
- Avocado linaweza kutengenezwa cream na ikaliwa kama ile uliyozowea kununua kwenye maduka ya Bakhresa. Hii inahitaji hatua fulani ili uweze kupata kitu ulichokikusudia.
- Avocado linaweza kupakwa kwenye mkate mfano wa siagi. Kama utapenda unaweza kutumia chumvi kidogo ili kuongeza ladha.
Kumbukeni unapoandaa vitu hivyo hapo juu ni lazima uzingatie usafi ukianzia wewe mwenyewe, vyombo utakavyotumia pamoja na matunda, siyo lazima upate matunda yote ili kukamilisha mchanganyiko ulioelezewa hapo juu, bali unaweza kuchukua baadhi kutegemeana na uwezo wako ili mradi tunda la msingi kama avocado lipo kwenye mchanganyiko wako. Matunda haya yapo karibu kila kona za mitaa ya Darisalama kwa wale waliopo jiji hilo, pia yanapatikana baadhi ya mikoa hapa nchini, hivyo siyo mpaka ushauriwe na daktari ndipo ule matunda, anza sasa kula matunda, japo moja kwa siku si haba.
Kwa wale watakaohitaji kujua maandalizi na matumizi ya avocado kwa ajili ya kutunza nywele au ngozi wanaweza kuwasiliana nami kupitia email zifuatazo: larkado@gmail.com au leofiderk@yahoo.com
Asante.
2FLAG