Tuesday, August 26, 2008

DOKEZO JUU YA MANENO "EAT AT YOUR OWN RISK"

Je, unafahamu kuwa watu tulio wengi tunachimbia makaburi yetu wenyewe kwa kutumia mikono, vijiko, visu na uma? Ni kwa nini nasema hivyo, kwasababu watu wengi tunapenda kula kila kitu kizuri tunachokiona kwa macho yetu na chenye ladha ulimini bila kujali athari za chakula chenyewe katika miili yetu. Tunakula vyakula vyenye sukari nyingi, mahanjumati yaliyokaangizwa kwa mafuta tusiyoyajua vizuri, chumvi nyingi ili tufurahishe ndimi zetu na vingine vingi vya namna hiyo kama wale wenzangu na mimi tunaopenda kwenda kujipumzisha ifikapo jioni au weekend katika maeneo fulani ya vimiminika huku tukipata nyama choma au kitimoto kwa wale walioamua kufumba macho.

Kumbuka, vyakula nilivyojaribu kuvitaja kwa uchache hapo juu ndiyo chanzo cha maradhi mbalimbali mwilini. Magonjwa ambayo ni rahisi kuyapata kutokana na ulaji wa vyakula kama hivyo ni artery, stroke, magonjwa yote ya moyo, kisukari, unene au kitambi ingawa watu wachache wanaipendelea hali hiyo ili nao waitwe au wafanane na mafisadi, na aina mbalimbali za magonjwa ya kansa.
Hebu fikiria, magonjwa mengi yamekuwa yakisababishwa na vimelea au wadudu mbalimbali wa magonjwa, lakini magonjwa niliyoyataja hapo juu hayahusiani na mdudu wa magonjwa isipokuwa mdudu wa ugonjwa kama huo ni wewe mwenyewe na chakula unachokula.
Hivyo ni vema kujikinga na vyakula nilivyotangulia kuvitaja kama vile vyenye sukari, vilivyopitia viwandani, vyenye chumvi nyingi, mafuta, protini nyingi, vinywaji baridi kama soda isipokuwa natural juice, vitafunwa au vitu vya kutafunatafuna kama maandazi, keki, donati n.k na pia tuepuke kula ovyo bila mpangilio. Hii ni kwa afya yako na faida yako na jamii inayokuzunguka. Haya, anza sasa, badilika. DON`T RISK YOUR LIFE, tunakupenda na bado tunakuhitaji. Usimtafute mchawi ukasema umerogwa pale utakapoanguka ghafla in case umepatwa na shinikizo la damu.

1 comment:

Anonymous said...

Asante kwa shule ...ila sijajua tusile kabisaa vyakula hivi au kama tukila tule kwa kiwango gani au katika interval gani na je kama nilishakula sana natakiwa kufanya nini..na je ni vyakula gani sasa mbadala maana hapo umetaja vyakula vingi ambavyo ndio milo yetu wengi..thanks more...Gluv100