Thursday, August 21, 2008

KARIBUNI WAPENZI WANABLOG


Kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kunijalia na kunipa uzima, ambapo pia amenipa uwezo huu wa kujumuika na wanajamii wenzangu katika safu hii ya blog maridhawa itakayokuwa inakupa elimu juu ya mambo mbalimbali ya afya yako.


Ndugu msomaji wangu, nimependa tushirikiane katika jambo muhimu la kiafya ambalo kimsingi watu wengi wanaona tabu kutumia japo muda kidogo kusoma mambo yanayowahusu moja kwa moja, lakini watu hao wapo radhi kupoteza muda mwingi kusoma na kuangalia mambo yasiyowaletea manufaa.


Blog hii itakuwa inakupatia elimu, mwongozo, ushauri wa kutumia mazao ya chakula kama mbogamboga na matunda kwa kinga na tiba dhidi ya maradhi mbalimbali yanayoweza kuathiri afya ya mwili wako. Ninaposema kinga au tiba kwa kutumia mazao ya chakula au mimea haina maana kuwa ni tiba za uganga wa kienyeji, bali ni kinga au tiba mbadala kwani chakula unachokula kila siku ndicho kitatumika kama kinga au tiba kama utaweza kukipangilia vizuri.


Kwahiyo ninawakaribisha wote katika blog hii mchango wenu wa mawazo mazuri ndiyo utatufikisha mahali pazuri, kwani nitatoa fursa pia kuongelea masuala mengine ya kijamii.


KARIBUNI.


2FLAG

4 comments:

2flag said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

Kama kweli umedhamiria kutoa elimu hiyo ya tiba asilia na matumizi ya vyakula kwa miili yetu utakuwa umetufanyia jambo la maana. Lakini isiwe nguvu ya soda ndugu yangu maana wengi walianza na wameshindwa kuendeleza blog zao.
OK, KILA LA HERI.

Anonymous said...

Good idea,Could become the best blog for now..karibu sana na tunasubiri na tutakuunga mkono...Kila la kheri kaka sijui ni dada...Gluv..gluv100@yahoo.com

Anonymous said...

Hongera sana kwa wazo zuri ambalo naamini blog yako itaweza kusaidia wengi kama itakuwa endelevu. Ni vyema tukumbuke sote kuwa hata hao waheshimiwa wakubwa wa ulaya wameshaona madhara ya kutumia artificial products na sasa wanatamani sana kuishi maisha asilia( natural life ) kwa kula vitu asilia. Ni vyema basi utoe elimu hii kupitia blog hii ili angalau wengi tuweze kuishi maisha asilia.